RISECHAMP DAY 2024

Tarehe 29 Juni kila mwaka shule yetu hufanya kumbukizi ya kuanzishwa kwake! Mwaka huu tarehe hiyo imeangukia Jumamosi, hivyo kumbukizi hiyo imepagwa kufanyika siku ya Ijumaa, tarehe 21 Juni 2024

Katika kuazimisha Risechamp Day 2024! mwaka huu tumepanga kushiriki katika kufanya usafi wa mazingira katika maeneo ya umma na utoaji vitendea kazi.

Maeneo tutakayoyafanyia usafi ni kama ifuatavyo: -

1) Zahanati ya Mpiji Magohe
2) Ofisi ya serikali ya mtaa Mpiji Magohe

Utoaji wa vitendea kazi: -
1) Tutatoa vifaa vya kusafishia mazingira kama mifagio n.k. kwa zahanati na ofisi ya serikali ya mtaa Mpiji Magohe
2) Tutaoa viti kwa ajili ya vikao/mikutano katika ofisi ya serikali ya mtaa Mpiji Magohe

Wahusika: - Walimu wote, baadhi wanafunzi, wazazi/walezi watakaopenda kushiriki nasi, na wengine wote wataopenda kuungana nasi siku hiyo.

Unaruhusiwa Kuchangia: -

Wataopenda pia kuchangia vifaa kama vile ufagio, mopers, gloves, kununua kiti/viti vya plastic n.k. wanakaribishwa sana kufanya hivyo. Tupigie 0762388399

Ratiba zitaanza saa 1:30 asubuhi.

Karibuni tuungane kuendelea kuigusa jamii inayotuzunguka!