• Call Us+255762388399
  • Login

Heri ya Sikukuu ya Muungano


Date: 26-Apr-2026



Wazazi na Walezi Wapendwa,

Tunapenda kuchukua fursa hii kuwatakia heri ya Sikukuu ya Muungano. Siku hii muhimu inatukumbusha thamani ya umoja, mshikamano, na amani ambayo ni msingi wa taifa letu.

Tunawahimiza kuendelea kuuenzi Muungano wetu na kuwafundisha watoto wetu umuhimu wa kuishi kwa upendo, kuheshimiana, na kudumisha amani katika jamii.

Asanteni kwa ushirikiano wenu wa kudumu katika malezi na maendeleo ya watoto wetu.

Tunawatakia Sikukuu njema yenye furaha na baraka tele.

Kwa niaba ya uongozi,

Mwalimu Mkuu