Date: 19-Jun-2026
Uongozi wa shule unawataarifu wazazi na walezi wote kuwa Holiday Package za wanafunzi kwa kipindi hiki cha likizo zimewekwa tayari kwa kupakuliwa.
Wazazi wanatakiwa kutembelea kiungo kilichotolewa hapa chini ili kupakua Holiday Package inayolingana na darasa la mtoto wako:
https://risechamp.ac.tz/site/share/R24ycmxKVmdDNWlHSFJwY2tNdk1KQT09
Baada ya kupakua package husika, mzazi anatakiwa:
• Kuchapisha (print) package hiyo.
• Kumwezesha mwanafunzi kufanya kazi zote zilizomo.
• Kufuatilia ili kuhakikisha kazi zimekamilika kikamilifu.
Holiday Package zote zitawasilishwa na kukusanywa siku ya kufungua shule. Zoezi hili ni sehemu ya kuimarisha ujifunzaji endelevu wa wanafunzi wakati wa likizo na kuwasaidia kujiandaa kwa muhula unaofuata.
Tunatoa shukrani kwa wazazi na walezi wote kwa ushirikiano wao katika kuendeleza taaluma na maendeleo ya watoto wetu.